STAY IN THE LOOP

Subscribe to our newsletter to receive the latest news

TALII THAMINI LINDA - KAMPENI

Tanzania ni nchi yenye mifumo ya kipekee ya asili pamoja na urithi mkubwa wa kitamaduni lakini Watanzania wengi hawajapata fursa ya kutalii na kuifahamu nchi yao. Kampeni ya Talii-Penda-Linda© inalenga kuwawezesha Watanzania wote kufurahia fursa hii na kuwafanya wajivunie na kwa msisimko mkubwa wagundue umiliki wao wa nchi hii ya kipekee.

Kwa kuwawezesha watu kuukumbatia urithi wa asili na kitamaduni wa nchi hii, kampeni hii inabeba mtazamo kuwa tunakilinda kile tunachokipenda, tunakipenda tu kile tunachokijua na tunakijua kile tu tunachofundishwa. Kupitia kuelimisha na kukuza ufahamu, kampeni hii inajenga maadili mapana ya ulinzi na utunzaji wa vivutio vyetu. Tukiwa na mabadiliko ya namna hii kifikra basi tunaweza kuondokana na mazoea ya muda mrefu yanayozuia juhudi za kupambana na matatizo kama vile ujangili dhidi ya wanyama pori ambao ni mojawapo ya rasilimali za kipekee hapa Tanzania.

Ili kufikia malengo haya tunaendesha Kampeni ya Talii-Penda-Linda© kwa kushirikiana na WMAs, TAWA, TANAPA na TTB chini ya Wizara ya Mali Asili na Utalii, na kwa kuungwa mkono na USAID PROTECT, UNDP, GIZ na wadau wengine wenye mtazamo huu ili kukuza shauku ya watu kupenda kufahamu zaidi juu ya mifumo ya viumbe hai ndani na nje ya mbuga kwa lengo la kukuza utalii wa ndani. Kampeni hii inatumia mfumo wa njia kadhaa za kufikisha ujumbe, kupitia makala fupi, mitandao ya kijamii, redio na mabango makubwa ili kupata mbinu rahisi, yenye unafuu na zinazoburudisha za kugundua mifumo ya viumbe hai wa Tanzania ndani na nje ya mbuga pamoja na thamani yake kwa ustawi wa mazingira na uchumi wa nchi.

Katika mifumo yote ya kufikishia ujuumbe, kampeni hii ina dhima zinazotambulika zilizojengwa kwenye maeneo na maudhui yale yale. Kampeni nzima imebebwa na nguzo mbili: moja ni kuendeleza ujumbe mkuu wa hazina za taifa kwa Watanzania na watu wengine hapa Arika Mashariki, na nyingine ikiwa ni matumizi ya nyenzo mbalimbali, maudhui, mikakati na njia za kuwasilisha ujumbe huu.

Maudhui yanayobebwa na mitandao ya kijamii yana uwezo mkubwa wa kuwasilisha taswira halisi kuliko njia zingine kwa kuwa na taarifa zenye kina na ubora wa hali ya juu. Maudhui huandaliwa ili yaendane na mtumiaji wa kila aina ya mtandao.

FACEBOOK

500

INSTAGRAM

300

TWITTER

400
TOP