MWISHO TUTATUNZA TU KILE TUNACHOKIPENDA

TUTAKIPENDA KILE TU TUNACHOKIELEWA

TUTAKIELEWA TU KILE TUNACHOFUNDISHWA[Baba Dioum]

TUNAKOTOKA

TANZANIA yenye utajiri
na utamaduni wa asili

Kukuza shauku kwenye utalii wa ndani na kujenga muamko wa kupenda kutunza utajiri wa asili

DIRA

Tunamshirikisha kila mtu kwa kuongeza mvuto
ili kukuza ari ya KUTALII nchini

MWELEKEO
WA MRADI

UANDAAJI-UTENDENEZAJI - WA FILAMU
Maeneo na maudhui

PREV
NEXT

MKAKATI UNAOTUMIA NJIA KADHAA ZA KUFIKISHA UJUMBE KUKUUNGANISHA NA MBUGA ZA AJABU ZA TANZANIA PAMOJA NA URITHI WAKE WA KITAMADUNI NA KIASILI

unaoendeswha na Nuru Agency

TTL KAMPENI

Kupitia Nuru Agency, watu wa Afrika Mashariki wanapatiwa fursa ya kugundua urithi wa asili na kitamaduni wa Tanzania [...]

soma zaidi

DIRA

Kuyashirikisha makundi mbalimbali ya walengwa katika namna ambayo itawafanya wabadili mitazamo yao ili kukuza shauku kwenye [...]

soma zaidi

MWELEKEO

Mkakati huu unatupeleka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mbuga za taifa na maeneo mengine yanayosimamiwa na wenyeji [...]

soma zaidi

SEHEMU "0"

Kipindi 0 ni hatua ya kwanza tu katika kuizindua kampeni ya TPL na kitatumika kuchangisha fedha kwa ajili ya mkakati mzima. [...]

soma zaidi

...WA UMMA
...TOKA TAASISI
...BINAFSI

SIGN UP to our NEWSLETTER

And keep up with the latest developments on the project, news, curiosity and Release schedules.

<KAMPENI YA MATANGAZO>

KWA KUSHIRIKIANA NA BODI YA UTALII TANZANIA (TTB), NURU AGENCY INAANDAA KAMPENI ITAKAYOTUMIA MABANGO MAKUBWA KUTANGAZA VIVUTIO VYA ASILI NA KITAMADUNI.

KIPENGELE HIIKI CHA KAMPENI HII KITAENDESHWA KWA MWAKA MMOJA NA KITALENGA MIJI MIKUBWA YA TANZANIA AMBAYO NI PAMOJA NA DAR ES SALAAM, MWANZA, ARUSHA, TANGA, ZANZIBAR, MOROGORO NA MBEYA NA SEHEMU NYINGINEZO MUHIMU ZA MIJINI.

PAMOJA NA MABANGO HAYA MAKUBWA, NURU PIA INAKUSUDIA KUWEKA MATANGAZO KWENYE LUNINGA 120 ZA KISASA ZILIZOPO KWENYE MADUKA MAKUBWA, MAHOSPITALI, KLINIKI, MAKANISA NA MAHOTELI.

<TV SERIES>

TPL NI MTIRIRIKO WA VIPINDI 16 VYA TELEVISHENI NA MTANDAO VYENYE UREFU WA DAKIKA 26 KILA KIMOJA. MTIRIRIKO HUU UNAONYESHA WANYAMA NA VIUMBE HAI VINGINE VYA PORINI, MANDHARI MBALIMBALI NA URITHI WA AJABU KWENYE MAENEO MBALIMBALI AMBAYO NI PAMOJA NA MAENEO YA USIMAMIZI WA WANYAMA PORI (WMAS), HIFADHI, MBUGA ZA TAIFA, MAENEO YA URITHI WA DUNIA YA UNESCO NA KWINGINEKO.

MTIRIRIKO WA TPL UNAHUSISHA WATANZANIA NA WATU WENGINE WA AFRIKA MASHARIKI KUTOKA NYANJA NA KADA MBALIMBALI ZA MAISHA UKIWAONYESHA WANAVYOTEMBELEA NA KUZURU MAENEO YA KUVUTIA HAPA NCHINI HUKU WAKIJIONEA WANYAMA NA VIUMBE WENGINE. KWA KUSHIRIKIANA NA WAFANYAKAZI WA MAENEO HAYA, WATAALAMU WA FANI YA VIUMBE NA WATAFITI WA KISAYANSI TUNAANGALIA KWA UNDANI CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA YA ASILI.

KILA KIPINDI KINA KISA CHAKE NA DHIMA. KWA UJUMLA, MTIRIRIKO HUU UNATOA UJUMBE MAHUSUSI UNAOSAIDIA KUJENGA AZMA YA KUUENZI NA KUULINDA URITHI WA TANZANIA. SEHEMU FUPI ZA VIPINDI HIVI ZENYE UJUMBE MUHIMU WA UTUNZAJI WA URITHI WA NCHI HII ZITAANDALIWA NA KUSAMBAZWA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII.

 

<Social Media>

TUNAENDESHA KAMPENI MAHUSUSI KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII AMBAYO NI PAMOJA NA FACEBOOK, INSTAGRAM NA YOU TUBE.

KWA KUITANGAZA KAMPENI HII KWA NJIA YA MITANDAO YA KIJAMII, MBINU NA HAMASA ZINASAMBAA KWA HARAKA HUKU ZIKIPANUA WIGO WA UFAHAMU JUU YA THAMANI YA URITHI WA TANZANIA NA KUCHOCHEA MIJADALA KUHUSU DHIMA MUHIMU.

<Radio Series>

VIPINDI VYA REDIO VINATENGENEZWA KWA AJILI YA BURUDANI PAMOJA NA KUELIMISHA NA MAKUSUDI YA KUKUZA UFAHAMU. TUNAANDAA VIPINDI VIPYA VYENYE UJUMBE TOFAUTI TOFAUTI UNAOWEZA KUINGIZWA KWENYE VIPINDI AMBAVYO VINAENDELEA.

REDIO ZA KIJAMII ZINAZOWEZA KUSIKIKA VIJIJINI ZITAPATIWA VIPINDI MAALUMU VINAVYOHUSISHA USHIRIKI WA VIKUNDI VYA KIJAMII VINAVYOTOKA KWENYE MAENEO YA USIMAMIZI WA WANYAMA PORI.

 

TOP